Janga la Corona, hakuna maambukizi ya ndani.

Serikali imeendelea kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa COVID 19 unaosababishwa na virusi vya CORONA, huku ikibainika hakuna maambukizi ya ndani, toka ugonjwa huo uingie nchini.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bibi. UMMY MWALIMU, akaweka wazi kuwa kati ya wagonjwa 13 waliobainika nchini, wote walipata maambukizi nje ya nchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Hamad Rashid, akawataka watanzania kuelewa lengo la serikali kuwaweka kwenye karantini wananchi na wageni wanaoingia nchini, ni kuzuia maambukizi, na siyo kuwanyanyasa.

Kupitia mkutano, imeazimiwa pia kutolewa elimu kwa wananchi kwa wagonjwa wanaopona wasinyanyapaliwe, kwa kuwa wataalamu wameshathibitisha hawezi kumbukiza mtu yeyote.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Magufuli apokea ripoti ya CAG na TAKUKURU.

Read Next

Naibu Waziri akagua mipaka kukabiliana na Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!