Kupambana na Virusi vya Corona maeneo ya masoko.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka wafanyabiashara wote wa Maduka maeneo yote ya Masoko pamoja na yale yanayotolewa huduma za jamii ikiwemo vituo vya Polisi kuweka Maji yenye dawa ili wananchi wote wanawe ili kuendelea kukabiliana na Maambukizi ya Mafua Makali yanayotokana na virusi vya Corona.

Bw,Lyaniva ametoa Agizo hilo baada ya kufanya Ukaguzi katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Temeke ikiwemo katika masoko,vituo vya Mabasi,ofisi za kata, vituo vya polisi na maduka kuangalia namna ya wafanyabiashara pamoja na wananchi wanavyoitikia wito unaotolewa na watalaam wa afya katika kukabiliana na corona.

Aidha Bw,Lyaniva alifanya Ukaguzi katika Maduka yanayouza Dawa pamoja na vitaka Mikono na kubaini kuwa baadhi yao wameendelea kuuza vitakasa Mikono kwa bei ya Juu na kuwaonya wauzaji wa Jumla na rejareja dhidi ya tabia ya kupandisha bei katika kukabiliana na corona.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Madaktari 1,000 walioajiriwa kupangiwa mikoa yenye uhitaji.

Read Next

Mfumo wa Taasusi wafunguliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!