Madaktari 1,000 walioajiriwa kupangiwa mikoa yenye uhitaji.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema upangaji wa madaktari watakaoajiriwa baada ya kutangazwa kwa nafasi 1,000 za ajira utazingatia uhitaji wa mikoa yenye uhaba wa watumishi hao.

Waziri Ummy ameeleza hayo jijini Dodoma katika mkutano na wanahabari ikiwa ni siku moja tangu serikali kutangaza nafasi za ajira kwa madaktari 1,000 kufuatia ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliyoitoa mapema mwanzoni mwa Februari alipokutana na madaktari na watumishi wa Afya.

Katika mkutano huo, Waziri Ummy amefafanua kuwa pamoja na nafasi hizo za kuajiri madaktari hao, wizara kwa kushirikiana na taasisi ya Benjamini William Mkapa, wameajiri watumishi wa afya wapatao 307 ambao wataongeza nguvu katika sekta ya afya ikiwamo kupambana na magonjwa ya mlipuko hususan Maambukizi ya virusi vya Corona katika halmashauri 68.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa Benjamin William Mkapa Foundation Dkt. Ellen Mkondya ameeleza kuwa tayari usaili umekamilika na kwamba watumishi hao watatakiwa kuripoti maeneo yao ya kazi Machi 27 mwaka huu.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mwandishi Mkongwe wa habari za michezo Asha Muhaji afariki.

Read Next

Kupambana na Virusi vya Corona maeneo ya masoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!