Mfumo wa Taasusi wafunguliwa.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imefungua mfumo wa kuchagua taasusi za kidato cha tano, ili wanafunzi waliofaulu mtihani wa kidatu cha nne mwaka jana, wachugue taasusi hizo kulingana na ufaulu wao.

Akitoa taarifa jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bw. Selemani Jaffo, akaweka wazi kuwa, ni wakati sasa kwa wanafunzi 135, 301 waliofaulu daraja la kwanza hadi la tatu, kufanya uchaguzi wa taasusi wanazotaka kwa kutumia simu janja au computer zilizo na mtandao, kabla ya kupangiwa shule na vyuo vya kati.

Waziri huyo wa nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), akatahadharisha kuwa nafasi iliyotolewa ni ya mwisho kwa wanafunzi na wazazi wao kuchagua taasusi za masomo wanayotaka kwenda kusoma kidatu cha tano na sita ama vyuo vya kati, kwa hiyo mfumo utakapofungwa, asitokee mtu kuleta malalamiko ya chaguzi zisizo sahihi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kupambana na Virusi vya Corona maeneo ya masoko.

Read Next

Rais Magufuli apokea ripoti ya CAG na TAKUKURU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!