Naibu Waziri akagua mipaka kukabiliana na Corona.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro ameeleza kuwa serikali itaendeelea kuruhusu upitishaji wa mizigo mipakani kuelekea nchi jirani na kusisitiza kuongezwa kwa uangalifu katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona katika maeneo yote ya mipaka.

Ameeleza hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa utayari wa kukabilina na mambukizi ya COVID 19 maeneo ya mipaka ambapo amekagua mpaka wa Burundi na Tanzania katika eneo la Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Amesema kuwa lazima biashara ziendelee hivyo umakini kwa wahudumu wa afya waliopo katika maeneo hayo ni muhimu kuimarishwa kwa wale watakao kuwa wanasafirisha mizigo hiyo na kufuata taratibu zilizowekwa .

Licha ya kuruhusu Magari ya mizigo kuvuka na kuingia nchi ya Burundi bado wafanyabiashara wadogo wadogo katika mpaka wa Manyovu wilayani Buhigwe wanaeleza kukumbana na changamoto ya kuharibika kwa bidhaa zao kutoka na katazo la kuvusha biashara ndogo kuelekea nchi ya Burundi.

Comments

comments

clement

Read Previous

Janga la Corona, hakuna maambukizi ya ndani.

Read Next

Njombe watenga vituo vya afya kukabiliana na Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!