Njombe watenga vituo vya afya kukabiliana na Corona.

Mkoa wa Njombe umeendelea kufanya maandalizi ya kukabiliana ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya COVID-19 kwa kutenga vituo maalumu vya aya vitakavyotumika kuwahudumia watu watakao bainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Akikagua vituo hivyo mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amesema miongoni mwa vituo vilivyotengwa ni pamoja na kituo cha afya Lyamkena kilichopo Halmashauri ya Mji Makambako, pamoja na zahanati ya kijiji cha Itunduma wilaya ya Njombe.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Deusidedit Kalaso amesema maandalizi yote yamekamilika, na wakati huohuo viongozi wa ngazi za vijiji wanasema wanendelea kuwashirikisha wananchi kuwapa elimu ikiwa ni pamoja na kudhibiti mikusanyiko kwenye vilabu vya pombe za kienyeji.

Wakati jitihada hizo zikiendelea kuchukuliwa na wizara ya afya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya COVID 19 serikali imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Naibu Waziri akagua mipaka kukabiliana na Corona.

Read Next

Uhispania yaongoza kwa maambukizi na vifo vya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!