Uhispania yaongoza kwa maambukizi na vifo vya Corona.

Taifa la Hispania limeendelea kukumbwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya Virusi vya Corona na kuwa Taifa la pili kuongoza kuwa na idadi kubwa ya Vifo vitokanavyo na Virusi hivyo ambapo mpaka sasa jumla ya idadi ya maambukizi imefika 56,188.

Nchini humo Idadi ya vifo imeongezeka kwa watu 738 ndani ya saa 24 kila siku na kufanya idadi ya vifo hivyo mpaka sasa kufikia 4,086, idadi ambayo iko juu zaidi ya Taifa la Italia.

Ripoti kutoka Mamlaka za Afya nchini Hispania zinaeleza kuwa Idadi ya maambukizi Uhispania imeongezeka mara tano ambapo karibu watu 27,000 wanatibiwa kila siku hospitalini.

Pamoja na mazuio mengi duniani bado virusi vya corona vinaonekana kuwa changamoto kubwa duniani ambapo mpaka sasa dunia ina wagonjwa 460,000 na vifo zaidi ya 20,000 huku watu zaidi ya 110,000 wakiwa wamepona ugonjwa huo.

Wakati huohuo nchi ya Marekani imejikuta kwenye hali tete baada ya kuthibitika kwa maambukizi 70,000 vya virusi vya corona mpaka sasa huku idadi ya vifo ikipanda na kufikia 1,050

Huko China katika jimbo la Hubei, ambako maambukizi ya virusi hivi vya corona vilianzia hali imeendelea kuwa shwari kutokana na kutokuwa na ongezeko la maambukizi mapya yaliyoripotiwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Njombe watenga vituo vya afya kukabiliana na Corona.

Read Next

Kamati za maafa ziungane na waratibu wa kukabiliana na Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!