Kamati za maafa ziungane na waratibu wa kukabiliana na Corona.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za Maafa katika ngazi za mikoa na wilaya ziungane na waratibu wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona waliopo kwenye maeneo yao.

Pia Waziri Mkuu amewasisitiza Watanzania waendelee kujikinga na ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanajiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na hata wakienda kwenye maeneo ya kutolea huduma kama sokoni, vituo vya mabasi wapeane nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.

Ametoa agizo hilo jana Alhamisi, wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa cha Kukabiliana na homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, na kuhusisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuratibu zoezi la kupeleka watu walioko kwenye karantini, wahakikishe wahusika wanafika kwenye hoteli walizozichagua huku Serikali ikifanya utaratibu wa kutenga maeneo ambayo watu watakuwa wanakaa bila gharama na ambayo yatakuwa na huduma zote muhimu.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu aliongeza wajumbe wawili ili waongeze nguvu katika kukabiliana na virusi vua corona ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uhispania yaongoza kwa maambukizi na vifo vya Corona.

Read Next

Wafanyakazi wa viwandani Kibaha waelimishwa kuhusu Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!