Wafanyakazi wa viwandani Kibaha waelimishwa kuhusu Corona.

Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya kata ya Visiga wilaya Kibaha mjini mkoa wa Pwani, wameanza ziara ya siku saba kutembelea maeneo ya viwanda na sehemu za biashara kila mtaa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na kirusi cha korona.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa zegereni Rashid Likunja pamoja na Afisa mtendaji wa kata hiyo Aloisia Nello wanasema zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mmoja wa wamiliki wa viwanda hivyo ameishukuru serikali ya kata ya Visiga kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wafanyakazi wa viwandani huku mmoja wa wafanyakazi hao wa viwandani akipongeza zoezi hilo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kamati za maafa ziungane na waratibu wa kukabiliana na Corona.

Read Next

Kampuni ya Uhuru Media yazindua gazeti lingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!