Kenya kufanyia binadamu majaribio ya Chanjo ya Corona.

Wanasayansi wa Kenya wameungana na wenzao wa kimataifa katika juhudi za kutafuta chanjo ya ugonjwa wa Covid-19, kwa kufanyia majaribio dawa tatu.

Majaribio ya chanjo hiyo yatafanywa kwa binadamu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.

Watafiti hao pamoja na wengine kutoka nchi mbalimbali wamekuwa mbioni kupata idhini ya kufanyia majaribio ya dawa aina tatu ikiwa ni pamoja na dawa ya Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura ya kutibu Covid-19, Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine pamoja na dawa aina ya Lopinavir/ritonavir, ambayo pia inatumiwa na wagonjwa wa HIV.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nation nchini Kenya mtafiti mkuu katika uchunguzi huo Dkt Loice Achieng Ombajo, ambaye ni mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta amesema kwamba kufikia sasa hakuna tiba ya Covid-19 anayopewa mgonjwa badala yake wagonjwa wanasadiwa kukabiliana na dalili zinazoonekana kama vile kuwa na homa kali na kuumwa na vidonda vya koo.

Wakati huo huo Wizara ya Afya nchini Kenya imesema idadi ya Maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19 imeongezeka na kufikia 535 baada ya ongezeko la Wagonjwa wapya 45.

Aidha Ongezeko hilo ni baada ya kufanya vipimo kwa watu 1,077 ndani ya saa 24 ikiwa ni ongezeko kubwa la maambukizi kuwahi kutokea ndani ya siku moja tangu Ugonjwa huo ulipoingia nchini humo.

Wizara hiyo imesema licha ya kuongezeka kwa maambukizi lakini wagonjwa takribani tisa wamepona na kufanya idadi ya waliopona corona mpaka sasa kufikia 182 huku idadi ya vifo ikiendelea kusalia 24.

Comments

comments

clement

Read Previous

Serikali yaelekeza fedha zitolewe kutatua changamoto ya Maji Dodoma.

Read Next

Ujerumani inatarajia kufungua biashara zote ifikapo May 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!