Ujerumani inatarajia kufungua biashara zote ifikapo May 11.

Marais wa majimbo nchini Ujerumani wanatarajia kukubaliana katika mazungumzo ya simu na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Jumatano wiki hii kuhusu kuanza kulegeza vizuizi vilivyowekwa kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona.

Kwa mujibu wa vyombo vya Habari nchini humo, Mamlaka katika majimbo hayo zinatarajiwa kutoa idhini ya kufungua tena maduka katika majimbo yote ya Ujerumani, kuanzia Mei 11 ambapo kwa sasa Biashara ndogo ndogo tayari zimeruhusiwa kufunguliwa tena kwa masharti ya kuheshimu hatua za kutokaribiana.

Mbali na Kufungua Biashara pia Mamlaka nchini humo zina nia ya kufungua tena shule za awali za chekechea ili kusaidia wazazi wengi wanaofanya kazi.

Ujerumani ilifikia hatua mpya Jumatatu wiki hii ya kuanza kulegeza vizuizi ikiwa ni pamoja na kufungua tena majumba ya makumbusho na sehemu za ibada na viwanda kadhaa vya magari, lakini wanasiasa nchini humo wamegawanyika kuhusu hatua hiyo kutokana na wengine kutokubaliana na suala hilo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kenya kufanyia binadamu majaribio ya Chanjo ya Corona.

Read Next

Jiji la Mwanza hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!