Mitaa ya Nairobi na Mombasa yawekewa amri ya kutotoka nje.

Wakazi wa maeneo ya Eastleigh mjini Nairobi na Old town mjini Mombasa nchini Kenya hawatoruhusiwa kutoka katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia saa moja usiku leo hii Jumatano 6 Mei, 2020.

Amri hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika maeneo mengine ya miji ya Nairobi na Mombasa huku wagonjwa wengine wapya 47 wakitangazwa na kufanya idadi ya maambukizi kufikia watu 580.

Katika wagonjwa wapya 47, wagonjwa 32 wanatoka Mombasa huku 11 wakitokea Nairobi. Wakazi wa Mtaa wa Bondeni mjini Mombasa wameonekana kukiuka masharti ya Afya yaliyotolewa na Serikali ambapo kati ya wagonjwa wapya 47, 18 wametokea kwenye huo mtaa na 5 wakitokea mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.

Waziri Kagwe ameoonya mitaa mingine kwamba itachukuliwa hatua kama hiyo iwapo itaendelea kukiuka maagizo ya Kiafya na kusababisha maambukizi ya kiwango cha juu.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mkakati wa kuifanya KMC FC kuwa timu ya mfano Nchini.

Read Next

Watumiaji wa maji washirikishwe usomaji wa Mita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!