Umoja wa Afrika kuchunguza ufanisi wa dawa ya mitishamba ya Madagascar.

Madagascar’s President Andry Rajoelina drinks a sample of the “Covid Organics” or CVO remedy at a launch ceremony in Antananarivo on April 20, 2020. “Covid Organics” or CVO is a remedy produced by the Malagasy Institute of Applied Research (IMRA) created from the Artemisia plant and supposedly help to prevent any infection caused by the new coronavirus Covid-19. (Photo by RIJASOLO / AFP)

Umoja wa Afrika (AU) unafanya mazungumzo na Jamuhuri ya Madagascar, ili kupata data za kiufundi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa ya mitishamba iliyotangazwa hivi karibuni ambayo ilidai inazuwia na kutibu Covi-19.

AU imesema kuwa Kamishna wa tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na masuala ya kijamii Amira El Fadil alifanya mazungumzo na Balozi wa Madagascar nchini Ethiopia Eric Randrianantoandro tarehe 30 Aprili na wameafikiana kuwa wataupatia maelezo muhimu Muungano wa Afrika kuhusu dawa za mitishamba.

Baada ya kupata maelezo ya Umoja huo kupitia kituo chake cha udhibiti wa magonjwa – (Africa CDC), kitatathimini data zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi katika tiba hizo asili dhidi ya virusi vya corona. Africa CDC ni taasisi ya Umoja wa Afrika inayosaidia nchi wanachama katika juhudi zao za kuimarisha mifumo ya afya na kuboresha uchunguzi, kukabiliana na dharura za magonjwa, kuzuwia na kudhibiti magonjwa.

Hata hivyo AU imesema kuwa tathimini yake ya madawa ya mitishamba itazingatia maadili ya kiufundi ya kidunia katika kukusanya ushahidi muhimu wa kisayansi kuhusu ufanisi wa mitishamba.

Hatua hii ya Umoja wa Afrika inakuja baada ya Rais wa Madagascar Andry Rajoelina kushiriki kikao cha AU cha wakuu waNnchi ambapo aliwafahamisha wenzake kuhusu dawa ya miti shamba ya Madagascar anayoamini inazuwia na kutibu virusi vya corona.

Hatua hiyo inawadia wakati ambapo Marais karibu wanne wa Afrika wamesema wanaagiza kiasi kikubwa cha dawa ya mitishamba iliyosemekana kupatikana huko Madagascar kuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya corona.Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Vifo vya corona Marekani vyazidi Elfu 70.

Read Next

Mkakati wa kuifanya KMC FC kuwa timu ya mfano Nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!