Raia 265 wa Nigeria waliokwama ughaibuni warejeshwa nyumbani.

Nigeria imeanza kuwarudisha nyumbani raia wake waliokwama katika mataifa ya kigeni kufuatia vizuizi vya usafiri vilivyosababishwa na mlipuko wa virusi vya Corona.

Kundi la kwanza ni Wanaijeria mia mbili sitini na watano ambao wamerejea nchini mwao kupitia mji wa Lagos Jumatano wiki hii wakitokea Dubai ambapo kundi la pili la watu 300 linitarajiwa kurejea nyumbani siku ya Ijumaa wiki hii wakitokea jijini London nchini Uingereza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria katika taarifa yake imesema kuwa raia wengine wa Nigeria wanatarajiwa kurudi nyumbani siku ya Jumapili wakitokea jijini New York nchini Marekani.

Baada ya kuwasili nyumbani, raia hao watalazimika kukaa karantini kwa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kwenda kuonana na wapendwa wao.

Raia hao wanarejea nyumbani, wakati huu nchi yao ikiendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Corona ambayo yamefikia karibu Elfu tatu na vifo vipya 98.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mtoto wa miaka 7 amefariki dunia baada ya kuzama kwenye mto.

Read Next

Silaha moja ya Kivita AK-47 na Gobole 21 zasalimishwa Katavi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!