Uingereza yaruhusu baadhi ya shughuli kuanza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kulegeza vizuizi vilivyowekwa nchini humo kufuatia mlipuko wa homa kali ya mapafu Covid-19 inayosababishwa na virusi vya corona, ambapo amesema kuanzia leo Mei 11, watu ambao wamekuwa hawawezi kufanya kazi wakiwa nyumbani, wanaweza kurejea makazini.

Aidha Bwana Johnson amesema kuanzia Jumatano wiki hii watu walio na jamaa zao majumbani wanaweza kutoka nje tena lakini kwa kuzingatia kwa umakini mkubwa tahadhari na kanuni za kujikinga na maambukizi ikiwemo ya umbali kati ya mtu na mtu. Hatua alizotangaza zinatoa ahueni kwa watu nchini humo baada ya shughuli nyingi kuathirika na uamuzi wa kuzifunga maarufu kama lockdown.

Amesema Serikali yake itatoa tangazo iwapo maduka yataanza kufunguliwa taratibu na iwapo wanafunzi wa shule za msingi wataweza kurudi shule kuanzia Juni Mosi sambamba na kutoa ruhusa ya watu kufanya mazoezi katika vituo vya mazoezi yaani Gyms.

Katika hatua nyingine China imeripoti kesi mpya 17 za Ugonjwa wa Covid-19 ambapo kesi 10 kati ya hizo ni maambukizi ya ndani, wagonjwa watano wakiripotiwa kutokea mji wa Wuhan zikiwa kesi za kwanza katika kipindi cha takriban mwezi mzima. Idadi iliyosalia imeripotiwa kutokea katika mji wa Jilin, ambao Mei 10 uliwekwa katika marufuku ya watu kutoka majumbani baada ya kuripotiwa kesi 10 za maambukizi.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wabunge wa CHADEMA wasiohudhuria vikao lawamani.

Read Next

Kigwangala aongoza wadau wa utalii kunusuru sekta hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!