Wanajeshi 19 wauawa kwa kombora la majaribio Oman.

Wanamaji 19 wameuawa na wengine 15 wakajeruhiwa katika tukio la ajali lililohusisha meli za kijeshi za Iran katika Ghuba ya Oman.

Vyombo vya habari vya Iran vimesema kwamba meli hiyo kwa jina la Konarak ilishambuliwa na kombora jipya lililokuwa likijaribiwa na meli ya kijeshi ya Frigate Jamaran wakati wa zoezi la kijeshi siku ya Jumapili.

“Siku ya Jumapili jioni wakati wa zoezi la wanamaji ambalo lilihusisha vyombo kadhaa vya wanamaji katika maji ya Jask and Chabahar, tukio moja lilifanyika likihusisha meli ya Konarak na kuwaua baadhi ya wanajeshi wa jeshi hilo” wanamaji hao walisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

Meli hiyo ilishambuliwa baada ya kupita katika eneo ambalo kombora hilo lilikuwa likirushwa baada ya kushindwa kupita mbali, runinga ya serikali ilisema katika tovuti yake.

Sio mara ya kwanza kwa jeshi la Iran kufanya makosa hayo. Mwezi Januari, kitengo cha ulinzi wa angani kilirusha kombora kutoka ardhini kikilenga kitu kisichojulikana, hatua ilioangusha ndege ya kampuni ya Ukraine na kuwaua abira wote waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Pemba yachukua hatua kali kwenye vita ya corona.

Read Next

Ferrari langalanga wakataa kumuongeza miaka mitatu Sebastian Vettel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!