Hafla ya kuapishwa serikali mpya ya Israel yaahirishwa.

Hafla ya kuapishwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Israel iliyotakiwa kufanyika hapo jana Alhamisi wiki hii imeahirishwa hadi jumapili,baada viongozi watakaoendesha serikali hiyo kukosa kukubaliana kuhusu Baraza la Mawaziri.

Waziri mkuu Benjamin Netenyahu anatarajiwa kuongoza kwa miezi 18 kabla ya mpinzani wake mkuu Benny Gantz kuchukuwa hatamu za uongozi, kwa mujibu wa makubaliano yao.

Netanyahu na Gantz, mkuu wa zamani wa jeshi nchini humo walitangaza mwezi uliopita kuweka kando tofauti zao na uadui na kujiunga pamoja kuiongoza nchi hiyo kupitia katika mzozo wa janga la virusi vya corona pamoja na hali mbaya ya kiuchumi.

Makubaliano hayo hata hivyo, yamesababisha kusambaratika kwa Chama cha Gantz cha Bluu na Nyeupe, na kuvunja ahadi yake ya kampeni ya kutohudumu chini ya Netanyahu, anaesubiri kupandishwa kizimbani kwa mashtaka ya rushwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Mkuu aridhishwa na maendeleo ya mradi wa SGR.

Read Next

TAKUKURU yaokoa Bilioni 11.3.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!