Visa vya corona Afrika vyafikia 79,931.

Hadi kufikia leo Bara la Afrika visa vilivyothibitishwa kuwa na virusi vya corona imefikia 79,931, vifo 2,640 na waliopona 30,226.

Kwa upande wa Bara la Afrika nchi inayoongoza kwa visa vya corona ni Afrika Kusini ikiwa na wagonjwa waliothibitishwa 13,524, vifo 247 na waliopona 6,083 ikifuatiwa na Egypt ikiwa na wagonjwa 11,228, vifo 592 na waliopona 2,799 huku Morocco ikiwa na wagonjwa 6,652, vifo 190 na waliopona 3,400.

Kwa nchi za Afrika Mashariki, Wizara ya Afya ya nchini Kenya hadi mapema leo hii imesema wagonjwa wapya 23 wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini humo na kufanya jumla ya visa vya corona Kenya kufikia 781 kutoka 758, vifo 45 na waliopona 284, huku nchini Uganda idadi ya visa vya corona vilivyothibitishwa ni 203, hakuna kifo kilichotangazwa kilichotokana na virusi vya corona na waliopona 63.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Visa vya corona vyazidi ongezeka Duniani.

Read Next

Serikali yawaonya wafanyabishara wanaohodhi sukari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!