Serikali ina mkakati wa kulinda ikolojia ya Wanyama.

Wizara ya maliasili na utalii imewaonya baadhi ya watu wanaovamia maeneo yaliyohifadhiwa kwa kuingiza mifugo na kuanzisha makazi jambo linaloathiri sehemu za ushoroba wa wanyama pori na kutishia ikolojia ya hifadhi ya tarangire na Serengeti.

Nibu waziri wa wizara ya maliasili na utalii Costantine Kanyasu Ameyasema hayo wakati akitembelea maeneo yaliyo hifadhiwa katika hifadhi ya jamii ya burunge iliyopo mkoani manyara ambapo amesema serikali ina mkakati wa kuweka mipaka ya kudumu ili kulinda ikolojia wanyama wasipotee.

Nae katibu wa hifadhi ya jamii ya burunge Benson Mwaise Amesema wamefanikiwa kupunguza vitendo vya ujangili ya uvamizi wa wafugaji ambao umekuwa ni changamoto kubwa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya babati ameeleza kuna umuhimu wa kuyalinda maeneo ya mazalia ya wanyama na njia zake ili kuwa na utalii endelevu.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kijana mbaroni akituhumiwa kumuua mama yake kikatili.

Read Next

Polisi Simiyu yamnasa aliyebaka mtoto wa miaka mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!