Tanzania yafunga mpaka wa Horohoro Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela amefunga mpaka wa Horohoro baada ya madereva 19 kutoka nchini Kenya waliopima Virusi vya Corona kugundulika wana maambukizi ya ugonjwa huo.

Ni ziara ya ghafla aliyoifanya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela katika eneo la mpaka wa Horohoro na kuona adha wanayopata madereva pamoja na wafanyabiashara wa mizigo hali iliyomfanya kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.

Nao Baadhi ya Madereva wakazungumzia changamoto ya upimaji wa virusi vya Corona sambamba na vipimo wanavyopimwa wakiwa nchini Kenya kutofautiana na vyaTanzania.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga BLASIUS CHATANDA akazungumzia hali ya usalama ilivyo katika maeneo hayo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mbunge Mtulia atoa ushuhuda alivyopona corona.

Read Next

Wananchi wapongeza hotuba ya Rais na maelekezo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!