Juhudi za umoja wa Ulaya kukwamua uchumi wake.

Ufaransa na Ujerumani zimependekeza kuanzishwa kwa mfuko wa Euro Bilioni 500 zitakazotumika kufadhili juhudi za kukwamua uchumi wa Umoja wa Ulaya kufuatia athari zilizosababishwa na janga la virusi vya Corona.

Viongozi wa nchi za Umoja huo wameamua kuweka kando tofauti zao za zamani na kutaka kuonyesha ushirikiano madhubuti baina yao ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wametangaza mpango huo wa kifedha usio wa kawaida baada ya mazungumzo kwa njia ya video.

Rais Macron amekiri kuwa Umoja wa Ulaya haukufanikiwa katika namna ulivyoanza kulishughulikia janga la virusi vya corona, wakati uchumi wake ukikumbwa na changamoto kubwa kabisa tangu Vita vikuu vya Pili ya Dunia hivyo unahitajika ushirikiano wa karibu zaidi wa nchi zinazounda umoja huo pindi yanapokuja masuala ya kiafya.

Taarifa yao imesema fedha hizo zitakazotolewa kupitia ufadhili wa mikopo kwa niaba ya Umoja wa Ulaya, zitapelekwa kwenye sekta na maeneo ya umoja huo yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Sherehe za kukabidhi kombe la Ubingwa Ligi Kuu Uingereza zitafanyika.

Read Next

Kenya imesema Tanzania ni ndugu, miamba ya Uchumi Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!