Rais Trump amesema endapo WHO haitafanya maboresho ya kazi yake anasitisha misaada.

Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuiondoa nchi yake katika Shirika la Afya Duniani, WHO kufuatia mzozo unaoendelea juu ya namna ya kushughulikia janga la virusi vya corona.

Trump ameonya kwamba ikiwa shirika hilo la WHO, halitafanya maboresho muhimu katika kazi yake katika muda wa siku 30, Marekani itatafakari upya uanachama wake katika shirika hilo la Afya Duniani na kusitisha kutoa michago yake.

Marekani imekuwa ikilishutumu Shirika la Afya Duniani kwa kuruhusu ugonjwa wa Covid -19 kushindwa kudhibitika na kuupuuzia hatari ya ugonjwa huo, ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

Mpaka sasa Corona tayari imeuwa zaidi ya watu 316,000 ulimwenguni kote, huku taifa la Amerika likiwa ndio lililoathiriwa zaidi na vifo vya zaidi ya watu 90,000 ambapo karibu watu milioni 1.5 wameambukizwa virusi vya Corona.

Comments

comments

clement

Read Previous

RC Makonda akagua Ujenzi wa Daraja la Tanzanite DSM.

Read Next

Serikali yapeleka gari la wagonjwa kituo cha Afya Lupilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!