RC Makonda akagua Ujenzi wa Daraja la Tanzanite DSM.

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amefanya ziara ya Ukaguzi wa Daraja la Kisasa la Tanzanite na kushuhudia Ujenzi wa Daraja hilo ukiendelea kwa kasi, ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika Oktoba Mwakani.

Kazi inayoendelea hivi sasa katika Ujenzi wa Daraja hilo ni kusimika nguzo ambazo zitaweza kubeba barabara itakayopita juu ya Maji usawa wa Mita tisa kutoka usawa wa bahari na kuweza kubadilisha mandhari ya Jiji la DSM.

Akizungumza na Waandishi wa habari Bw. Makonda amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo lakini pia usimamizi makini wa mshauri mwelekezi wa mradi huo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo wa Dar es Salaam akatumia fursa hiyo kuwataka wenye Mahoteli, maduka na biashara mbali mbali zilizofungwa kutokana na hofu ya ugonjwa wa Corona kuzifungua na kuendelea na huduma kama ilivyokuwa mwanzo, lakini pia wakazi wa DSM waliokimbilia Mikoani kwa hofu ya kuambukizwa Covid-19 kurejea kwa kuwa hali ya Jiji inaendelea kuwa Shwari.

Kuhusu Sukari Bw. Makonda amewataka wafanyabiashara wanaosambaza na kuuza sukari kwa Bei ya Rejareja kuzingatia Bei elekezi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali ya Mkoa wa DSM itaendelea kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya wafanyabiashara watakaoendelea kukaidi maagizo ya Serikali.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi watatu TEMESA.

Read Next

Rais Trump amesema endapo WHO haitafanya maboresho ya kazi yake anasitisha misaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!