Serikali yapeleka gari la wagonjwa kituo cha Afya Lupilo.

Kituo cha afya ya Lupilo kilichopo wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kimepokea gari la wagonjwa (Amburance) iliyotolewa na serikali kwa ajili ya kituo hicho huku mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga akipongeza hatua ya serikali kufunga kifaa cha ungalizi wa gari hilo maarufu kama CAR Track katika kuhakikisha gari hilo linafanya kazi iliyokusudiwa na serikali katika kusaidia huduma za afya kwenye eneo hilo la Lupilo.

Katika hafla hiyo ya kukabidhiwa gari ilitoa furaha kwa wakazi wa lupilo na wafanyakazi wa kituo cha afya ambapo mbunge wa jimbo la ulanga goodluck mlinga amesema ni wakati wa kushukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutokuwa wabagudhi katika nafasi ya vyeo wakati wa kuhudumia wananchi wake na kutumia nafasi hiyo kuwataka wananchi hao kulitunza gari hilo.

Hapa wananchi wanaonyesha jinsi walivyofuraishwa na upatikanaji wa Ambulance hiyo huku mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya ulanga amesema ni utekerezaji wa ilani ya uchaguzi katika kuboresha huduma za afya.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Trump amesema endapo WHO haitafanya maboresho ya kazi yake anasitisha misaada.

Read Next

Wakulima wa pamba Maswa warejeshewa fedha walizoibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!