Sherehe za kukabidhi kombe la Ubingwa Ligi Kuu Uingereza zitafanyika.

Mtendaji Mkuu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Richard Masters ametangaza kuwa sherehe za kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi hiyo zitafanyika kama ilivyo desturi ya kumtangaza bingwa, japokuwa kwa mwaka huu itakuwa chini ya uangalizi maalum.

Masters amesema shughuli hiyo ni lazima kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendeshaji wa ligi ambazo zinawatendea haki wachezaji na viongozi wa timu washindi ambar wametoa jasho hadi kupata mafanikio hayo.

Kipekee amewataja Liverpool ambao kwa mujibu wa hesabu wananafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo, akisema wanahitaji kupata ushindi kwenye mechi mbili pekee ili wachukue ubingwa ambao wameuwinda kwa miaka 30 sasa.

Timu za ligi kuu nchini Uingereza, zimeanza kuitikia wito wa kurejea mazoezini kwa kuwaruhusu wachezaji kwa mafungu mafungu, ikiwa ni maandalizi kwa mÈchi za ligi hiyo ambazo zinatarajiwa kuanza Juni 12.

Comments

comments

clement

Read Previous

Tume yatakiwa kushughulikia malalamiko ya walimu.

Read Next

Juhudi za umoja wa Ulaya kukwamua uchumi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!