Madereva 19 wa Tz waliotangazwa na Kenya kuwa na Corona, Hawana.

Madereva 19 wa Malori wa Tanzania waliopimwa Ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya na kukutwa na Maambukizi wamekutwa hawana maambukizi ya Ugonjwa huo mara baada ya kurudia vipimo katika maabara kuu ya taifa hapa nchini.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo imebainisha hayo ambapo amesema ili kujiridhisha na majibu ya Madereva wa Tanzania waliokutwa na Ugonjwa wa Covid-19 kwa mujibu wa Mamlaka za Kenya walichukua sampuli 19 za madereva hao na kuzipima tena na kukuta hawana maambukizi.

Taarifa hiyo imesema kufuatia ongezeko la kesi za Ugonjwa huo katika maeneo ya mpakani Mkoa huo umeanzisha utaratibu wa kuwapima madereva wa malori wanaotokea Kenya kuingia nchini kupitia Mpaka wa Namanga.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ya Bwana Gambo, amesema Sampuli za madereva kutoka Kenya zilichukuliwa tarehe 14,16 na 18 ya mwezi Mei ambapo kati ya madereva 44 waliopimwa Mei 14, madereva 14 kati yao walikutwa na maambukizi huku 30 wakiwa salama na kati ya hao madereva 14 madereva 11 ni raia wa Kenya, mmoja kutoka Uganda na uraia wa madereva wengine wawili umehifadhiwa.

Aidha Majibu ya Sampuli 23 za Mei 16 yalithibitisha madereva 10 wote kutoka Kenya walikutwa na Virusi vya Corona na wengine 13 walikutwa hawana. Bwana Gambo amesema sampuli za Mei 18 bado zinafanyiwa vipimo na majibu yatatolewa yakishapatikana.

Mrisho Gambo amesema baada ya majibu ya vipimo hivyo Mkoa wake umejiridhisha kuwa hizo ni mbinu za Kenya kuua Soko la Utalii la Arusha na Tanzania kwa ujumla na hivyo kulazimika kuchukua hatua za kuhakikisha madereva wa malori hawapiti mpakani bila kupimwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wananchi wahimizwa kujenga tabia ya kunawa mikono.

Read Next

Zoezi la Uchaguzi Mkuu Burundi lafanyika licha ya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!