Rais Magufuli aagiza ufumbuzi wa migogoro mipakani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dk. John Pombe Magufuli, amewataka wakuu wa mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandishi Isack Kamwelwe kukutana mara moja na viongozi wa Kenya, ili kwa pamoja wamalize tofauti zilizojitokeza mipakani katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid 19.

Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.

Rais Magufuli ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi mkoani Singida aliposimama njiani akitokea Chato mkoani Geita, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania na Kenya ni nchi jirani zenye udugu ndani yake, hivyo hatokubali kuona udugu wa nchi hizo ukitetereka kwa sababu ya Corona.

Rais Magufuli amesema wananchi hawapaswi kuendelea kuishi kwa hofu ya Corona na kutoa wito kwa Watanzania kutumia siku tatu kuanzia Ijumaa kumshuruku Mwenyezimungu kwa kuitikia sala na dua za Watanzania kuwaondolea ugonjwa wa Covid 19 unaoitesa dunia kwa sasa.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amevitaka vyama vya ushirika wa mazao (AMCOS) kuacha kuwanyonya na kuwaibia wakulima stahiki zao na kwamba hayupo tayari kusikia wakulima wananyonywa kwa kisingizio cha AMCOS.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwananchi mmoja kulalamika mbele ya Rais Magufuli kwamba hajalipwa fedha zake za choroko alizouza, ambapo Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi kushughulikia malalamiko hayo na ahakikishe wakulima wote wanaodai wanalipwa fedha zao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watalii kuanza kuwasili hapa Nchini Julai 2.

Read Next

Kimbunga Amphan chaikumba India.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!