Zoezi la Uchaguzi Mkuu Burundi lafanyika licha ya Corona.

Raia nchini Burundi leo Mei 20 wanapiga kura katika uchaguzi mkuu, zoezi litakalowezesha kumpata mrithi wa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Rais Pierre Nkurunziza.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya miaka mitano ya mvutano ambao ulichochewa na kile kilichoelezewa Rais Nkurunzinza kutaka kuongeza awamu ya tatu ya uongozi wake, hali iliyosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine zaidi ya laki nne kukimbia nchi hiyo.

Raia wa taifa hilo wameonekana katika misururu mirefu tangu kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura mapema asubuhi, kufanya maamuzi kwa njia ya kidemokrasia kumchagua rais wa taifa hilo, wabunge na madiwani. Zoezi hilo linaendelea licha ya kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya corona ambapo Burundi imeamua kuendelea ili kufanikisha zoezi hilo la kupata viongozi .

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Madereva 19 wa Tz waliotangazwa na Kenya kuwa na Corona, Hawana.

Read Next

Watalii kuanza kuwasili hapa Nchini Julai 2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!