Wakulima wa pamba Maswa warejeshewa fedha walizoibiwa.

Shilingi Milioni 232 fedha za Wakulima wa Pamba Wilayani Maswa Mkoani Simiyu ambazo zilitafunwa na Viongozi wa Vyama Vya Msingi Vya Ushirika (AMCOS) Wilayani humo katika msimu wa mwaka 2019-2020, kutokana na kuzitumia kwa kuchezea mchezo wa upatu na kukopeshana zimeendelea kurudishwa kwa Wakulima baada ya Viongozi waliyokamatwa na Jeshi la Polisi kufikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), katika Wlaya hiyo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Seif Shekalaghe wakati akizungumza na Wakulima wa Pamba katika Kijiji cha Nguliguli, akiwa katika Muendelezo wa kuhamasisha Wakulima kufungua akaunti za Benki kama yalivyo maelekezo ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ili wakulima hao walipwe fedha zao kupitia akaunti na kupunguza ubadhirifu wa fedha za wakulima uliokuwa ukifanywa hapo awali na Viongozi wa Amcos.

Kwa sasa msimu wa pamba kwa mwaka 2020/2021 unatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali yapeleka gari la wagonjwa kituo cha Afya Lupilo.

Read Next

Wananchi wahimizwa kujenga tabia ya kunawa mikono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!