Watalii kuanza kuwasili hapa Nchini Julai 2.

Bodi ya utalii nchini TTB imesema ndege zenye kubeba watalii zinatarajiwa kuanza kuwasili tena hapa nchini Julai pili mwaka huu huku wadau wa sekta hiyo yakiwemo mahoteli yakiwa katika mchakato wa kurejesha huduma zao kama ilivyokuwa awali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TTB Devotha Mdachi ameyapongeza mashirika ya uwakala wa utalii kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuanza mchakato wa kuleta watalii ambapo amesema watalii ambao awali walitarajiwa kuwasili nchini kati ya Januari na Februari mwaka huu sasa wanatarajiwa kuanza kuingia nchini mwezi wa saba kupitia mashirika ya ndege ya Uturuki na Emirates.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kwa sasa vikao kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo mazingira salama kwa watalii vinaendelea huku baadhi ya wadau ikiwemo sekta ya mahoteli zikiwa zimefungua kambi za watalii kwenye hifadhi za wanyama.

Kabla ya shughuli za utalii kusitishwa kwa muda kutokana na janga la corona, zaidi ya watalii elfu kumi walikuwa tayari kuwasili nchini kupitia mawakala wa utalii kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Israeli, China na Jamhuri ya Chek.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Zoezi la Uchaguzi Mkuu Burundi lafanyika licha ya Corona.

Read Next

Rais Magufuli aagiza ufumbuzi wa migogoro mipakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!