Ndege ya Ethiopia yasafirisha samaki kutoka Mwanza.

Sera ya Taifa ya Tanzania ya viwanda iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya tano, imeanza kuleta majibu katika ushindani wa biashara za kimataifa, baada ya ndege kubwa kutoka nchini Ethiopia kutua Jijini Mwanza, kwa ajili ya ubebaji wa minofu ya samaki tani 19.62 kuelekea Ubelgiji.

Ndege hii kubwa aina ya Dream Liner kutoka nchini Ethiopia, ni mara yake ya kwanza kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jijini Mwanza, ambapo ubebaji wa shehena hii unatajwa kutimiza matakwa ya sera ya viwanda, kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Akishuhudia usafirishaji wa shehena ya minofu ya samaki, Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema safari hizi za kimataifa zitafungua fursa za upatikanaji wa fedha za kigeni, kupitia sekta ya viwanda na usafiri wa anga.

Jiji la Mwanza ni kitovu cha kibiashara kwa nchi za maziwa makuu, huku umuhimu wake ukidhihirika katika jumuiya ya kimataifa, baada ya mataifa mbalimbali kuanza kutumia fursa ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza katika shughuli za kibiashara.

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kusafirisha shehena ya tani za minofu ya samaki kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jijini Mwanza, kuelekea kwenye baadhi ya nchi za jumuiya ya ulaya,

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Nzige, Covid-19 na mafuriko kitisho kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki.

Read Next

Tanzania na Kenya zafikia muafaka wa Mipaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!