Gwaride la kumpongeza Askari aliyemuokoa mtoto kutoka shimoni, avishwa Cheo.

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera limefanya gwaride maalum la kumpongeza na kumvisha cheo mmoja wa askari wake aitwaye Danis Minja ambaye hivi karibuni alitumbukia ndani ya shimo la choo na kufanikiwa kumuokoa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyedaiwa kutumbukizwa humo na mtu ambaye hajatajwa.

Tukio hilo lililoangaziwa pakubwa na mitandao ya kijamii lilitokea mapema wiki hii katika Kata ya Murgwanza wilayani Ngara ambapo askari huyo aliyekuwa na cheo cha Constable na sasa Koplo kulazimika kuingia mzima mzima kwenye tundu la choo ili kumtoa mtoto huyo.

Gwaride la kumpongeza limefanyika mjini Bukoba zilipo ofisi za zimamoto ambapo askari huyo amesema mbali na kufanya kazi hiyo kulingana na mahitaji ya kazi yake lakini aliguswa kama mzazi kuona mtoto anaelekea kufia ndani ya shimo.

Mapema Kamanda wa kikosi hicho mkoa wa Kagera Inspect Shaban Dawa amesema ni utaratibu wa jeshi hilo kupongeza watumishi wake wanaofanya matendo ya kishujaa kama alilofanya askari huyo na kwamba amepandishwa kutoka constable kuwa koplo.

Hadi tunakwenda mitamboni hali ya mtoto ilikuwa inaendelea vizuri na amelazwa katika hospitali ya Omurugwanza wilayani Ngara huku taarifa rasmi za nani aliyemtupa kwa shimo hilo zikiwa bado hazijulikani vema.

Comments

comments

clement

Read Previous

Madiwani Sita Upinzani wahamia CCM.

Read Next

Mbunge Lijualikali wa Kilombero aikimbia CHADEMA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!