Mbunge Lijualikali wa Kilombero aikimbia CHADEMA.

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mkoani Morogoro kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Peter Lijuakali ametangaza kuachana na chama hicho kwa madai ya kukwazwa na baadhi ya mambo yanayoendelea kwenye chama hicho, licha ya kutotangaza kuhamia chama chochote lakini akaendelea kusisitiza kauli yake aliyoitoa bungeni kwamba endapo Chama Cha Mapinduzi CCM kitaridhia kumpokea atakuwa tayari kuhamia kwenye chama hicho na kuchapa kazi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari na kueleza kuwa hata kama hatapokelewa na chama chchote hatakuwa tayari kurudi CHADEMA kutokana na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama hicho ikiwemo kukosekana kwa uwazi wa matumizi ya fedha za chama.

Lijuakali ameyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na kugeuza matumizi ya fedha za chama ikiwemo michango iliyokuwa inatolewa na wabunge kwa kukatwa posho zao kwa lengo la kufanya maendeleo ya chama lakini jambo la kushangaza ni kwamba fedha hizo zimekuwa zikitumika kinyume na makubaliano na kunyimwa nafasi ya kuhoji.

Aidha ameeleza kuwa zipo hoja mbalimbali zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambazo amesema kimsingi hazina mashiko kwani uamuzi aliouchukua hakulazimishwa na mtu na endapo atahamia CCM atakwenda kufanya kazi yoyote kama alivyokuwa akifanya akiwa CHADEMA bila kuchagua.

Comments

comments

clement

Read Previous

Gwaride la kumpongeza Askari aliyemuokoa mtoto kutoka shimoni, avishwa Cheo.

Read Next

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 hospitali yapungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!