Tanzania na Kenya zafikia muafaka wa Mipaka.

Mawaziri wa Sekta ya Uchukuzi kutoka Tanzania na Kenya wamekutana katika Mpaka wa Namanga Upande wa Tanzania kutatua changamoto ya kibiashara na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili katika kuvuka mpaka wa nchi moja kwenda nyingine.

Katika mkutano huo wamekubaliana mpaka wa Kenya kufunguliwa kwa magari ya mizigo kupita na madereva wa kila nchi watapimwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID – 19 katika nchi anayotoka na atakuwa na cheti ambacho atakionyesha katika mpaka na cheti hicho kitatumika kwa siku 14.

Mkutano uliochukua Zaidi ya saa nne katika kujadili namna ya kutatua changamoto iliyopo katika mpaka Tanzania na Kenya.

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Anna Mgwira anasema makubaliano hayo yamewasaidia wafanyabiashara wa pande zote mbili katika kusafirisha bidhaa.

Katika mkutano huo umeudhuriwa na wakuu wa Makatibu wakuu kutoka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano -Sekta ya Uchukuzi,Katibu Mkuu Mambo ya Nje ,wakuu wa Mikoa kutoka Arusha,Kilimanjaro,Mara,Tanga na Mwanza.

Ikumbukwe mkutano huu umafanyika kutokana na Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Hivi karibuni akiwa katika ziara yake Mkoani Singida.

Comments

comments

clement

Read Previous

Ndege ya Ethiopia yasafirisha samaki kutoka Mwanza.

Read Next

Watalii kuanza kuja nchini kuanzia Juni Mosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!