Watalii kuanza kuja nchini kuanzia Juni Mosi.

Wakati dunia ikiwa katika taharuki ya ugonjwa wa COVID-19, Kamishna wa uhifadhi wa shirika la hifadhi za taifa Tanzania, TANAPA Dkt. Allan Kijazi amesema baada ya ugonjwa huo kuonekana kupungua hapa nchini na sehemu mbalimbali duniani, Shirika hilo limejipanga vyema kuanza kupokea watalii watakaofika nchini kuanzia Mwezi June mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi ya taifa ya TANAPA iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha Dakta Kijazi amesema shirika hilo limejiandaa kupokea wageni ambao wameshaonesha nia ya kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini kuanzia mwezi June ambapo watahakikisha wanaboresha huduma za afya ili wageni watakaokuja waondoke salama ili kuvutia watalii wengine.

Dkt. Kijazi pia amesema shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa wafanyakazi wake na litaendelea kutoa elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia miongozo yote inayotolewa na serikali.

Hivi karibuni wadau wa utalii wakiongozwa na waziri wa maliasili na utalii dakta Hamis Kigwangala walikutana jijini Arusha kwa siku mbili kujadiliana namna bora ya kuweka mikakati ya kufungua tena sekta ya utalii katika zama hizi za tishio la ugonjwa wa COVID 19 baada ya sekta hiyo kuonekana kuathiriwa vibaya kutokana na ugonjwa huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Tanzania na Kenya zafikia muafaka wa Mipaka.

Read Next

Madiwani Sita Upinzani wahamia CCM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!