Familia ya watu 30 yanusurika kifo kwa kutumia maji yenye sumu.

Watu 30 wa familia moja wa jamii ya kifugaji katika kijiji cha Mkusi Kata ya Kapenta Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa wamenusurika kufa baada ya maji ya kisima wanayotumia kunywa na matumizi mengine ya nyumbani ikiwamo kunyweshea mifugo kuwekwa sumu na kusababisha vifo vya mifugo ng’ombe 15, punda 1, paka na bata wanane.

Hofu imetanda kwa familia ya ndugu Elias Juma baada ya kunusurika kufa kwa kutumia maji yaliyotiwa sumu na badala yake wamekufa mifugo wa familia hiyo kama anavyoeleza mwenyekiti wa kijiji cha Mkusi pamoja na baba wa familia iliyopata mkasa huu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina Msaidizi wa polisi Justine Masejo watuhumiwa wawili wamekamatwa watafikishwa mahakamani taratibu zitapokamilika.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Manaibu Waziri wawili watembelea mradi wa umeme wa JNHPP.

Read Next

UDP yatangaza kuunga mkono Rais Magufuli Uchaguzi Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!