UDP yatangaza kuunga mkono Rais Magufuli Uchaguzi Mkuu.

Chama cha siasa cha UDP, leo kimetangaza rasmi kwamba hakitaweka mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na badala yake kitamuunga mkono Rais aliyeko madarakani Mhe. Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, endapo CHAMA CHAKE CHA MAPINDUZI kitampitisha kuwa mgombea wake wa kiti cha urais.

Mwenyekiti wa chama hicho cha UDP Bw. JOHN MOMOSE CHEYO, amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, kwamba hatua hiyo inalenga kutambua utendaji madhubuti wa Mhe. Rais Magufuli katika kutekeleza miradi mingi ya maendeleo na kuisimamia serikali kwa ufanisi.

Akizungumza kwa kutoa takwimu, Bw. Cheyo amesema kutokana na utendaji huo, zaidi ya hospitali 75 zimejengwa, zahanati 400, barabara za kupitika zaidi ya kilomita 3,000 nchini kote, na hivyo UDP kama chama cha siasa hakioni sababu ya kuweka mgombea ambaye ataweza kukinzana na maendeleo hayo.

Kuhusu nafasi nyingine za kugombea, Bw. Cheyo amesema UDP imetangaza kuanza rasmi kwa zoezi la uchukuaji wa fomu katika nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge na kwamba mwisho wa uchukuaji fomu utatangazwa baadae, baada ya kamati kuu ya chama hicho kukaa na kuamua.

UDP kinakuwa chama cha pili cha siasa chenye usajili wa kudumu kutangaza kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, baada ya chama cha TANZANIA LABOUR (TLP) kinachoongozwa na Bw. AUGUSTINE LYATONGA MREMA kufanya hivyo mwezi uliopita.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Familia ya watu 30 yanusurika kifo kwa kutumia maji yenye sumu.

Read Next

Upungufu wa mafuta ya petroli waikumba miji ya Ruvuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!