Upungufu wa mafuta ya petroli waikumba miji ya Ruvuma.

Kati ya vituo kumi na mbili vinavyouza mafuta katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ni kituo kimoja ambacho kinatoa huduma hiyo na kusababisha Shughuli za usafiri kwenye mji wa huo kumesimama kutokana na uhaba wa petroli hali ambayo imemlazimu mkuu wa wilaya Pololet Mgema kuingilia kati kwa kumuagiza mkuu wa polisi wilaya kuwatafuta baadhi ya wafanyabiashara wanaosadikika kuficha.

Baadhi ya madereva pikipiki (bodaboda) na wale wanaotumia magari wanasema tatizo limekuwa kubwa ,kwani ni siku ya tatu sasa huduma ya mafuta katika wilaya ya Songea imekuwa changamoto ,huku mmoja wa wafanyabiashara akikili kuwepo kwa uhaba huo.

Mkuu wa wilaya ya Songea Bwana Pololet Mgema akiwa katika kituo cha kuuzia mafuta amesema tayari kuna kikosi kazi kinachunguza ili kubaini tatizo baada ya kubainika mafuta kufishwa.

Kwa ujumla Hali ya mafuta aina ya petrol katika mkoa wa Ruvuma imekuwa kubwa.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

UDP yatangaza kuunga mkono Rais Magufuli Uchaguzi Mkuu.

Read Next

Vijana wa Kitanzania waendelezwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!