Wenye viwanda vya Mkonge wataka Ulinzi wa Soko.

Pamoja na juhudi zinazofanywa Wizara ya Kilimo chini ya Bodi ya Mkonge na Taasisi ya utafiti wa kilimo nchini TARI katika kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima na jinsi ya utumiaji wa mbegu bora zinazoweza kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa lakini bado wamiliki wa viwanda nchini wameomba serikali kuangalia namna ya kupambamba na uingizwaji wa kamba za plastic ambazo zimeonekana kushusha soko la ndani la kamba za mkonge na kupunguza juhudi za serikali kukabili uharibifu wa mazingira.

Akiongea na Channel Ten Meneja wa kiwanda cha kuchakata Mkonge cha Ambone Spinning Mill LTD Freddie Semwaiko ameiomba serikali kungalia mara mbili juu ya uwingizwaji wa bidhaa hiyo ya kamba kutoka nje ya nchi huku Meneja wa kiwanda cha Sagera Estase LTD Imani Mshana amesema mpango wa serikali katika kurudisha hadhi ya kilimo cha Mkonge kama ilivyo zamani kutapandisha uchumi wa nchi.

Huyu ni Husein Hamis ni mwajiliwa wa kiwanda cha mkonge miaka 40 iliopita ameonyesha kufuraishwa na hatua za serikali katika kurudisha hadhi kilimo cha mkonge hapa nchini kwani kutaweza kuongezeka kwa viwanda vya kuchakata mkonge na mashamba na kutoa nafasi kwa watu wengi zaidi akiwemo mtoto wake kuweza kupata ajira.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Shilingi 100 yatosha kukupa Mamilioni na Parimatch Casino.

Read Next

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Siku na tarehe ya Uchaguzi Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!