Serikali kununua ndege kubwa ya mizigo.

Serikali inatarajia kununua ndege kubwa ya mizigo, ili kuokoa gharama na muda wa usafirishaji wa minofu ya samaki kwenda nje ya nchi, zinazowakabili wamiliki wa viwanda vya kusindika minofu hiyo Kanda ya Ziwa.

Ahadi hiyo ya serikali imetolewa Jijini Mwanza na mkurugenzi wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) Ladslaus Matindi, baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea uwanja wa ndege wa Mwanza na viwanda vya kusindika minofu ya samaki vya Nature’s Fish na Omega.

Hatua ya serikali kutaka kununua ndege hiyo imefuata, kutokana na uhaba wa ndege za usafirishaji wa minofu ya samaki kwenda nje ya nchi, jambo linalosababisha adha ya usafiri kwa wamiliki wa viwanda vya kusindika minofu ya samaki.

Mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Emmanuel Koroso, amesema kutokana na tatizo hilo, serikali imeanza kufanya mazungumzo na nchi mbalimbali za kigeni, ili kuruhusu usafirishaji wa mizigo kwa kutumia ndege zilizopo.

Tatizo la usafirishaji wa minofu ya samaki kutoka nchini kuelekea nje ya nchi limechomoza, baada ya kuwepo ongezeko la tani za usindikaji wa minofu hiyo kwa siku katika viwanda mbalimbali kanda ya ziwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

UWT Dar es Salaam kupiga kura ya maoni kesho.

Read Next

Watuhumiwa 15 washitakiwa kwa makosa ya mtandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!