UWT Dar es Salaam kupiga kura ya maoni kesho.

Hapa jijini DSM, Mchakato wa kuwapata wagombea Ubunge kupitia Viti Maalum kwa Mkoa wa DSM unatarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa PTA-Sabasaba jijini DSM ambapo zaidi ya wagombea 252 wamejitokea katika kinyang’anyiro hicho.

Katibu wa UWT Mkoa wa DSM Bi. Grace Crispin Haule akizungumza na Channelten amesema Utaratibu wote umekamilika ambapo katika nafasi za Viti Maaalum waliojitokeza ni wagombea 162 huku katika nafasi hiyo wakihitajika wagombea wawili pekee kwa mkoa wa DSM.

Aidha nafasi nyingine zitakazogombaniwa ni pamoja na kundi la Watu wenye ulemavu, wafanyakazi, na vyuo vikuu ambapo katika Makundi hayo inahitajika nafasi moja moja kwa kila kundi…

Wakati huo huo M/kiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Harold Maruma amesema amepokea Ujumbe kutoka kwa Watanzania wanaoishi Ujerumani juu ya kutaka kuanzisha Tawi la CCM katika Mji wa Munich nchini humo ili kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Amesema Watanzani hao wameguswa na maendeleo yanayoendelea kutokea nchini lakini pia utaratibu wa kura za maoni ambao walioshuhudia moja kwa Moja kupitia kituo cha channel ten.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Rais Magufuli aitaka TAKUKURU kujitathimini.

Read Next

Serikali kununua ndege kubwa ya mizigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!