Watuhumiwa 15 washitakiwa kwa makosa ya mtandao.

Watuhumiwa 15 wa makosa ya kimtandao wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu jijini DSM kujibu tuhuma zinazowabili.

Kati ya watuhumiwa hao kumi na watano ambao wote ni wakazi wa Ifakara wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, wawili ni mawakala wa mitandao mbalimbali ya simu, ambapo wanatuhumiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari na Juni mwaka huu.

Makosa mengine yanayowakabili ni pamoja na kula njama na kufanya udanganyifu wa kujipatia kipato, kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo huku wakijua wazi kuwa ni kosa kisheria, kusambaza ujumbe kwenye mitandao mbalimbali ya simu bila ridhaa ya mpokeaji wakiwa na nia ya kumlaghai na kuchapisha taarifa za uongo zikiwa kwenye ujumbe mfupi zinazosema umepokea kiasi fulani cha fedha wakiwa na nia ya kudanganya.

Aidha kosa jingine ni kutotoa mabadiliko ya mtumiaji wa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine kwa mtoa huduma wa mtandao husika jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kwa upande wa mawakala, wao wanakabiliwa na kosa la kutumia taarifa za mteja vibaya kwa kusajili namba ya simu ya mtu mwingine.

Watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali kununua ndege kubwa ya mizigo.

Read Next

Ubalozi mdogo wa China mjini Houston waamuriwa kufungwa na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!