Machafuko ndani ya ZANU PF Zimbabwe, Jeshi laonya,lasema liko tayari kuingilia kati yasipokomeshwa

chiwenga-mujuruSD

Jeshi la Zimbabwe limeonya kuwa liko tayari kuingilia kati mtifuano wa wenyewe kwa wenyewe unaoendelea ndani ya chama tawala cha Zimbabwe African National Union-Patriotic FrontZANU PF kinachoongozwa na Rais Robert Mugabe,kufuatia hatua ya kumfuta kazi makamu wa Rais wa nchi hiyo Emmerson Munangagwa,wiki iliyopita.

Katika taarifa zake nadra mkuu wa majeshi wa nchi hiyo,Constantino Chiwenga,ametoa wito wa kukomeshwa mara moja mzozo ndani ya chama unaolenga kuwaondoa wanachama wa ZANU PF,walioshiriki ukombozi wa nchi hiyo la sivyo jeshi litaingilia kati.

Mkuu huyo wa majeshi amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi halitasita kuwashughulikia wale wote wanaojaribu kuleta dhihaka na waliopambana kuleta ukombozi wa nchi hiyo.

Machafuko ndani ya ZANU PF,yamefuatia kitendo cha Rais Mugabe,kumfuta kazi Makamu wa Rais na waziri wa zamani wa ulinzi na usalama,lengo likiwa ni kumsafishia njia mkewe Grace Mugabe,kumrithi madaraka yake.

Comments

comments