Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa boti katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Jumamosi iliyopita, imefikia zaidi ya 30, wakati huu zoezi la kutafuta miili zaidi ikiendelea.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Zura Ganyana amesema kuwa hadi sasa watu walionusurika ni 27 huku zaidi ya 60 wakiwa bado hawajapatikana.

Sababu za kuzama zinaelezwa kuwa huenda ni idadi kubwa ya watu na hali mbaya ya hewa katika Ziwa hilo aidha Ripoti za awali zinasema kuwa, boti hiyo haikuwa imesajiliwa na haikuwa na kibali maalum cha kufanya safara za maji.

Comments

comments