Wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki wilayani Arumeru wametakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi ambao watajitolea kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo hilo ambalo bado lipo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na viongozi wa mila wa kabila la wameru maarufu kama washili kwa lengo la kujadili ni kwa namna gani wananchi hao wameupokea uamuzi wa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kumfutia ubunge , mbunge wao Joshua Nasari.

Mmoja wa viongozi maarufu jimboni humo generali mstaafu Merisho Sarakikya amesema baada ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano Job Ndugai kutangaza rasmi jimbo la Arumeru mashariki kuwa wazi ni vyema wakazi wa eneo hilo wakajitafakari upya wakati wa kuchagua aina ya viongozi wanaowataka kwa manuafaa ya wananchi walio wengi.

Machi 14 spika wa bunge alimuandikia barua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji Kaijage kutaarufu kuwa mbunge wa jimbo la Aru,meru mashariki Joshua Nasari amepoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge baada ya kushindwa kuhudhuria vikao vya bunge mara tatu mfululizo bila ruhusa ya spika.

Comments

comments