Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo alikuwa miongoni mwa waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa marehemu Paulina Kassama Seleman ambaye ni mama mzazi wa mbunge wa viti maalum Geita Vicky Kamata.

Ibada ya kuaga mwili wa marehemu mama Paulina Kasama Selema ambaye pia ni dada wa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristi Ndikilo imefanyika katika kanisa la mtakatifu Petro jijini DSM Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete naye amehudhuria ibada hiyo ya kuaga mwili wa mama mzazi wa mbunge Vicky Kamata. Wakati huo huo Rais Dkt.[…]

Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetupilia mbali ombi la aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama cha wanachi CUF Maalim Seif Sharrif Hamad alilofungua mwaka 2016 la kuitaka Mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Msajili wa vyama vya siasa kumtambua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa M/kiti wa Chama cha wananchi CUF.

Uamuzi wa kutupilia Mbali kesi hiyo Uliofanywa na Jaji Benhaj Masoud ulizingatia sheria ambapo anayepaswa kufungua kesi dhidi ya Prof.Lipumba na wenzanke 12 ni Mjumbe wa bodi au M/kiti wa Bodi ya Udhamini na siyo Maalim Seif Shariff Hamad ambaye hana Mamlaka ya kufungua kesi ya Kumpinga Prof.Lipumba. Akizungumza na waandishi wa habari Wakili aliyekuwa[…]

Jumla ya vituo Arobaini na Sita Elfu kati ya mia moja thelathini na moja elfu vya kutolea huduma za maji vijijini vimebainika kutokuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi hivyo kusababisha malengo ya serikali ya kuhakikisha upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 85 kutofikiwa.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na katibu mkuu wizara ya maji Prof. Kitila Mkumbo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kisayansi la siku mbili linaloambatana na maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa kuanzia tarehe 18 hadi 22 ya mwezi huu. Akizungumza kando ya kongamano hilo Prof. Mkumbo amesema hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu serikali ilikuwa[…]

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameziagiza taasisi za Umma na sekta binafsi, kuachana na tabia ya urasimu wa utoaji wa taarifa vyombo vya habari, ili kuiwezesha Serikali ya awamu ya tano kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Akifungua kikao kazi cha maafisa mawasiliano wa Serikali Jijini Mwanza, kinachoongozwa na kauli mbiu isemayo “utoaji wa habari sahihi kwa wakati, ni chachu ya kuifikia Tanzania ya kipato cha kati”, amesema kuwa Serikali haitaifumbia macho tabia hiyo katika baadhi ya sekta. Njoo kesho au mimi si msemaji, hizi ni baadhi ya kauli zilizopigwa marufuku na[…]

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Idai kilichokumba maeneo mbalimbali nchini humo kikiwa na mwendo kasi wa kilomita 177 kwa saa.

Mpaka kufikia leo imeripotiwa kwamba watu 65 ndio walipoteza maisha Mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga hicho. Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake mashariki ya kati ili kurejea nchini mwake kutokana na janga hili. Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walioko,hali inahofiwa kwamba huenda inaweza ongeza[…]

Kesi na Tatu ya mwaka 2019 inayowakabili washitakiwa watatu Mariana Malekela, Edwin Malekela na Kalistus Ndiungwa kwa kosa la mauaji ya Mtoto Rachel Malekela mwenye umri wa miaka saba ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Matembwe, Tarafa ya Lupembe mkoani Njombe kwa imani ya kishirikina imetajwa Leo na kuahirishwa hadi April Mosi, Mwaka huu kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Washitakiwa hao watatu wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Jamesi Mhanusi, ambapo kesi yao ikiwa imetajwa kwa mara ya tatu na kuahirishwa katika mahakama hiyo huku washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha mashitaka wa Serikali, Nura Manja ambaye alitaja shauri hilo na kuiomba mahakama itaje tarehe nyingine hadi Aprili Mosi,[…]

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameyashinikiza makampuni ya mitandao ya kijamii kutoa maelezo juu ya namna mshambuliaji alivyoweza kurusha moja kwa moja mitandaoni shambulizi lake kwa muda wa dakika 17, na video ya shambulizi hilo kuenea mitandaoni kwa saa kadhaa.

Aidha Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa nchi hiyo inajipanga ndani ya siku kumi kuimarisha sheria ya umiliki wa bunduki ili kudhibiti matumizi holela ya silaha ambazo zimekuwa tishio kwa usalama wa jamii Leo kumekuwepo ulinzi mkali katika mji wa Christchurch nchini New Zealand, wakati shule na shughuli za kibiashara zikifunguliwa kwa mara ya kwanza tangu[…]

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji wa Wizara ya Madini, Mikoa na Kamati za Ulinzi na Usalama wasimamie vyama vya wachimbaji wadogo na wahakikishe uongozi wake hauingiliwi na wachimbaji wa kati kwa lengo la kuepusha migogoro.

Aidha ameiagiza Wizara ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wa madini kuandaa Mpango kazi mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko la madini la Geita ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo hayo jana jioni Machi 17 wakati[…]

Wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki wilayani Arumeru wametakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi ambao watajitolea kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo hilo ambalo bado lipo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na viongozi wa mila wa kabila la wameru maarufu kama washili kwa lengo la kujadili ni kwa namna gani wananchi hao wameupokea uamuzi wa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kumfutia ubunge , mbunge wao Joshua Nasari. Mmoja wa viongozi maarufu jimboni humo generali mstaafu Merisho[…]

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gorge wilayani Rufiji mkoani Pwani imeelezea kuridhishwa na hatua za awali za utekelezaji mradi huo.

Katika eneo hilo kamati hiyo imejionea kazi za miundombinu-wezeshi ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na nguzo za umeme kwenye mradi huo ambao unaratajiwa kutumia zaidi ya shilingi trilioni 6.5 na kuzalisha umeme megawati 2,115 utakapokamilika. Akiongea mara baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya madini na nishati kutembelea eneo la mradi wa kuzalisha umeme[…]