Wakandarasi Wanawake waomba Miradi Mikubwa.

Wakandarasi wanawake nchini wameiomba serikali kupunguza masharti ya upataji wa zabuni katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ili nao waweze kuongeza ushiriki wao utakaochangia kuleta mabadiliko ya kimaendeleo nchini lakini pia ukuaji wa kipato chao. Hadi sasa bado kuna gepu kubwa la upataji wa zabuni kwa wakandarasi wanawake jambo linalochangia[…]

Ushirikiano kati ya Polisi na Raia wasaidia kupunguza Uhalifu.

Jeshi la Polisi limesema hali ya Uhalifu nchini inaendelea kupungua kutokana na wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo pamoja na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hususan katika utoaji wa taarifa zinazosaidia kuwafichua wahalifu na kudhibiti matukio ya Uhalifu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Operesheni Nchini Kamishna wa Polisi[…]

Majenerali Wastaafu JWTZ Waagwa.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ limewaaga majenerali wastaafu 9 wa jeshi hilo ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida ambao licha ya kustaafu wataendelea kulishauri wakiwa nje pindi itakapohitajika kufuatia uzoefu walionao katika kipindi chote walicholitumikia. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, lililofanyika Mgulani, jijini Dar es Salaam Mkuu wa[…]

Mamlaka Nchini Sudan zimeamuru Kufungwa Shule zote Kuanzia leo.

Mamlaka nchini Sudan zimeamruru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo hadi pale zitapotangaza kufunguliwa. Tangazo hilo limekuja siku moja kufuatia vifo vya waandamanaji sita wakiwemo wanafunzi watano, waliouawa Jumatatu wakati wa maandamano katika mji wa Al-Obeid, katikati mwa nchi hiyo. Vifo hivyo pia vilisababisha kusitishwa kwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika jana kati ya viongozi wa waandamanaji[…]

Jiandikisheni Katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jaffo amewataka watanzania kutumia muda uliotengwa kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura waweze kutumia fursa ya kumchagua kiongozi atakayewaongoza katika serikali za mitaa huku akisisitiza kwamba wasikubali kumchagua kiongozi atakayetoa rushwa ili kupata nafasi ya[…]

Serikali yasisitiza Uhifadhi wa Misitu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN amesema upo umuhimu wa kuzisimamia kikamilifu sheria, sera na matamko mbalimbali ya uhifadhi misitu ili kuilinda kutokana na uharibifu unaoongezeka kila mwaka. Mama SAMIA ameeleza kuwa uharibifu wa misitu umeongezeka kwa kasi ambapo takwimu za mwaka 2018 za chuo kikuu cha SOKOINE[…]