Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa familia, kufuatia kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo ametoa pole kwa familia, kufuatia kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Magufuli amekwenda nyumbani kwa Marehemu Salasala Jijini Dar es Salaam na kukutana na familia ikiongozwa[…]

Serikali yaendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara.

Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha zaidi sekta binafsi ili iweze kutoa mchango wake unaohitajika kwa uchumi wa taifa. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa[…]

Rais Dkt. Magufuli amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi TTCL.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bwana Mohammed Abdallah Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es Salaam imesema kuwa Bw. Mtonga anachukuwa nafasi ya Dkt. Omari Rashid Nundu ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti[…]

Waziri Jaffo amefika eneo la daraja la Mbuchi linalounganisha kijiji cha Mbwela.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMESEMI Seleman Jaffo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga daraja la Mbuchi linalounganisha kijiji cha Mbwela anafika eneo la mradi mapema wiki ijayo kuendelea na kazi baada ya kubaini kuwepo kwa ubabaishaji katika[…]

Rais Dkt. Magufuli leo anatarajiwa kuwaapisha Waziri wa viwanda na biashara na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuwaapisha Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe,Charles Kicheere na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Edwin Mhede Ikulu jijini Dar es salaam. Baada ya shughuli ya kuapisha,Mhe.Rais Magufuli atashuhudia tukio la Kampuni ya[…]

Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa.

Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vya kuzalisha mifuko mbadala hatua ambayo itasaidia kuwapatia kipato na hatimaye kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya mifukpo hiyo. Kutokana na madhara kadha wa kadha yanayotokana na matuimizi ya mifuko ya plastic ikiwa ni pamoja na kusababisha[…]

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma.

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma,reli ambayo inatarijiwa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa ukanda wa kusini kupitia sekta ya usafirishaji ambapo pamoja na usafirishaji wa bidhaa zingine chuma na makaa ya mawe yanatarajiwa kusafirishwa kwa wingi kupitia reli hiyo. Hapa ni[…]

TBS imeanza mkakati wa kubaini wazalishaji wa vifaa vya ujenzi wanaokiuka masharti ya leseni ya ubora.

Shirika la viwango Tanzania TBS limeanza mkakati wa kubaini wazalishaji wa vifaa vya ujenzi wanaokiuka masharti ya leseni ya ubora waliopewa ambapo maafisa wa shirika hilo wanachukua sampuli za vifaa hivyo kwa lengo la kupima ubora wake na kwamba bidhaa itakayogundulika haina ubora mzalishaji atachukuliwa hatua. Akizungumza mkoani Mtwara wakati wakikagua vifaa vya ujenzi kwenye[…]