Kesi ya Lulu, Mahakama kutoa Majumuisho kesho

Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam,kesho inatarajiwa kutoa majumuisho ya kesi inayomkabili Msanii Elizabeth Michael ”maarufu kama Lulu, ya mauaji ya bila kukusudia kufuatia upande wa utetezi kufunga ushahidi wake. Hatua hiyo ya mahakama chini ya Jaji Sam Rumanyika, inafuatia wakili wa upande wa mtuhumiwa Peter Kibatala,kuiambia mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi wao na Read more about Kesi ya Lulu, Mahakama kutoa Majumuisho kesho[…]

Ugaidi Afrika, Marekani yaombwa kuingilia kati

Makamanda wa ngazi ya Juu katika jeshi la Marekani wameshauri taifa hilo kuongeza nguvu na fedha zaidi kukabiliana na vikundi vyenye msimamo mkali wa kigaidi barani Afrika . Kuuawa kwa wanajeshi wanne wa Marekani nchini Niger kumeelezewa kuzidisha haja ya Marekani kuweka msukumo zaidi kukabiliana na makundi yenye msimamo mkali wa kigaidi, hasa baada ya Read more about Ugaidi Afrika, Marekani yaombwa kuingilia kati[…]

Biashara ya Mahindi kutoka nchi jirani na Rukwa, Serikali yapiga marufuku wafanyabiashara kuyaingiza kwa magendo

SERIKALI mkoani Rukwa imepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara kuingiza mahindi mkoani humo kutoka nchi jirani ya Zambia kwa kutumia njia za panya na kuyauza kwa bei ya chini inayosababisha mahindi yaliyolimwa nchini kukosa soko na kuikosesha serikali mapato. Ziara ya ghafla ya mkuu wa mkoa wa Rukwa katika mpaka usio rasmi wa Safu umebaini kushamiri Read more about Biashara ya Mahindi kutoka nchi jirani na Rukwa, Serikali yapiga marufuku wafanyabiashara kuyaingiza kwa magendo[…]

Sakata la wanafunzi kugongwa Songwe lashika kasi

SAKATA la kugongwa na vyombo vya moto kwa wanafunzi wanaosoma katika shule zilizopo pembezoni mwa barabara mkoani Songwe,limezidi kushika kasi na kuzua taharuki kwa wazazi na walimu ambao wameiomba serikali kuweka alama za barabarani ikiwemo matuta ili kulinda usalama wa wanafunzi. Licha ya kituo hiki kutangaza mara kwa mara uwepo wa wanafunzi kugongwa kutokana na Read more about Sakata la wanafunzi kugongwa Songwe lashika kasi[…]

Mwaka mmoja katika kuifufua ATCL, Wafanikiwa kupunguza hasara kwa mwaka 2016/17

Shirika la Ndege la Tanzania ATCL limefanikiwa kupunguza hasara iliyopatikana mwaka wa fedha 2015/16 ya shilingi billioni ishirini hadi kufikia shilingi billioni 4.4 katika mahesabu yake ya mwaka wa fedha 2016/17 ikiwa ni mwaka mmoja tu toka serikali ianze rasmi jitihada za kulifufua shirika hilo Octoba mwaka jana. Aidha maboresho hayo yamechangia kukuwa kwa biashara Read more about Mwaka mmoja katika kuifufua ATCL, Wafanikiwa kupunguza hasara kwa mwaka 2016/17[…]

Chama tawala cha China, Xi Jinping ashinda muhula Mwingine

Rais wa China Xi Jinping ametangaza safu mpya ya uongozi wa kamati kuu ya chama Tawala cha kikomunisti wakati akianza muhula wa mpya wa miaka mitano, akilenga kuimarisha ustawi na kupanua ushawishi wa taifa hilo kimataifa . Kama ilivyotarajiwa amepewa muhula mwingine kufuatia mkutano wa kwanza wa kamati kuu mpya iliyochaguliwa wakati wa mkutano mkuu Read more about Chama tawala cha China, Xi Jinping ashinda muhula Mwingine[…]

Majeshi ya Iraq yaanza kuikomboa Raqqa

Majeshi ya Iraq yanajitayarisha kuanzisha mashambulizi kukomboa eneo la mwisho la ardhi ya Iraq linalokaliwa na kundi linalojiita dola la Kiislam IS. Dola la Kiislam limekuwa likirudi nyuma kutokana na mashambulizi makali toka makundi yanayoungwa mkono na Marekani na mashambulizi toka Jeshi la Syria. Ngome ya Raqqa ilikombolewa na majeshi yanayoungwa mkono na Marekani, na Read more about Majeshi ya Iraq yaanza kuikomboa Raqqa[…]