BALOZI WA JAPAN AKAGUA MRADI WA DARAJA LA GEREZANI

Balozi wa Japan hapa nchini INICHI GOTO amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Gerezani unaojengwa na mkandarasi kutoka kampuni ya SUMITOMO MITSUI Construction Company (SMCC) ya Japan kwa kushirikiana na wakala wa barabara nchini TANROADs.

Daraja hilo jipya litachangia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam hususan kwa wakazi wa Kurasini, Mbagala na Kigamboni.

Mwakilishi wa JICA, SATORU MATSUYAMA amesema daraja hilo jipya la Gerezani litaboresha usafirishaji katika jiji ambapo mabasi ya mwendowa haraka yatapita pamoja na reli ya kisasa ya standard gauge (SGR) ambayo itapita chini ya daraja hilo.

Aidha amesema daraja hilo litarahisisha usafiri wa kwenda na kutoka bandari ya Dar es salaam hivyo kuchochea kasi ya kukuza uchumi ikizingatiwa kuwa bandari hiyo inahudumia mizigo kwa asilimia 40 inayokwenda nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na Rwanda

Naye balozi wa Japan hapa nchini amesema hiyo ni moja ya mashirikiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na Japan na kwamba mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi katika kanda ya afrika mashariki na kati.

Comments

comments